Ahmed amesema malengo yetu yatafikiwa endapo tutakuwa pamoja na tunapaswa kuanza Jumamosi kwa kujitokeza kwa wingi kwa Mkapa kuhakikisha tunapata pointi tatu.
"Simba ina malengo ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na tunaanza Jumamosi kwa kucheza na ASEC na mashabiki tunawsomba kujitokeza kwa wingi kuwapa hamasa wachezaji," amesema Ahmed.
Kwa upande wake Mzaramo Simba amesema Simba ndio timu yenye mashabiki wanaojielewa na hawawezi kuitupa timu yao kwahiyo amewaomba waje kwa wingi Jumamosi.
"Najua kuna magari mawili ya mashabiki kutoka Arusha wanajiandaa kuja na wengine kutoka sehemu nyingine mnapaswa kuja kwa Mkapa tuipe sapoti timu yetu," amesema Mzaramo.
Kwa upande wake Key Mziwanda amesema "Mwanasimba wa kweli hawezi kuacha kuisapoti timu yake kwa namna yoyote kwahiyo Wanasimba wenzangu tukutane Jumamosi tukachukue pointi zetu tatu kutoka kwa ASEC."