Simba Sports Club
News

Mashabiki Mwanza wahamasiahwa kununua jezi Orijino

10 Oct 2025

Ziara hiyo ambayo ilianza Jumatatu Oktoba 6 imefanyika katika maeneo ya Kisesa, Buhongwa, Nyamagana, Machinjioni na Nzega

Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally ameendelea kuwasisitiza Wanasimba kununua jezi orijino ili kuiwezesha klabu kupata mapato ambayo yatasaidia uendeshaji wa timu.

Ahmed amesema Wanasimba wanatakiwa kuwa na mazoea ya kununua vitu halisi ili kuinufaisha klabu lakini pia ni kutengeneza furaha yao wenyewe.

Advertisement

Aidha Ahmed ameendelea kusema ahadi zilizotolewa na Mzabuni Jayrutty utekelezaji wake unatokana na mauzo mazuri ya jezi hivyo kila mwanasimba ana wajibu wa kuhakikisha anakataa uuzwaji wa jezi feki.

"Ndugu zangu leo tupo hapa Mwanza lengo letu moja tu kuhamasisha Wanasimba wenzetu kununua jezi mpya na orijini na kuacha kununua jezi feki kwakuwa hazisaidii kitu chochote kwenye timu wala klabu."

"Tunajua kila shabiki anatamani kuiona timu yetu ikifanya vizuri, hilo halitawezekana kama hakutafanyika uwezekaji na ili uwekezaji ufanyike ni lazima pesa ipatikane ambayo sehemu yake ni kwenye mauzo ya jezi hivyo kila mmoja wetu awe balozi wa hili," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story