Simba Sports Club
News

Manula: Tunazidi kukua katika Soka la Afrika

26 Apr 2022

Manula amesema kila mwaka tunapanda viwango vya uchezaji kitu ambacho anaamini baada ya miaka michache ijayo tutatikisa Bara la Afrika.

Manula ameongeza kuwa changamoto tunazopata katika michuano ya Afrika zinazidi kutujenga na kutuimarisha ambapo msimu ujao tutakuwa bora zaidi ya ilivyo sasa.

Advertisement

"Mimi ninaamini tunazidi kukua siku hadi siku. Tumefika robo fainali mara nne lakini safari hii tumetolewa kwa penati. Msimu ujao tutakuwa bora zaidi. Tumeimarika na changamoto za Afrika tunazijua," amesema Manula.

Back to homepage
Share this story