Simba Sports Club
News

Manula nje miezi minne, kurejea nchini Jumapili

2 Jun 2023

Manula amefanyiwa upasuaji huo Jumanne Mei 30 baada ya kupata majeraha katika mchezo wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Ihefu FC uliopigwa Aprili 7, mwaka huu.

Leo jioni Manula ameruhusiwa kutoka hospitali na kesho mchana ataanza safari ya kurejea nyumbani ambapo atafika Jumapili.

Daktari wa timu Edwin Kagabo ambaye yupo naye nchini Afrika Kusini amesema baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali, Manula ataingia kwenye sehemu ya pili ya matibabu yake.

Advertisement

Dk. Kagabo amesema sehemu ya pili ya matibabu itakuwa kufanya kliniki ya mazoezi ya viungo (Physiotherapy) kwa kwa utaratibu maalumu ili apone vizuri.

"Manula ameruhusiwa kutoka hospitali leo na kesho tutaanza safari ya kurudi nyumbani. Anatakiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi minne ili kupona kabisa."

"Katika kipindi hiki Manula atapaswa kuhudhuria kliniki ya mazoezi ili kumsaidia jeraha lake lipone vizuri," amesema Dk. Kagabo.

Back to homepage
Share this story