Simba Sports Club
News

Manula Mchezaji bora wa Mwaka BMT

17 Mar 2023

Manula amewapiku walinzi Mohamed Hussein na Shomari Kapombe alioingia ingia nao fainali ya kinyang'anyiro hicho ambao wote wanatoka kwenye kikosi chetu.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mratibu wa timu, Abbas Ally kutokana na mlinda mlango Aishi kuwa kambini kujiandaa na mchezo wa kesho wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Horoya.

Advertisement

Aishi amedaka asilimia kubwa ya mechi zetu pamoja na timu ya Taifa kwa mwaka mzima huku akiwa kwenye ubora mkubwa.

Back to homepage
Share this story