Simba Sports Club
News

Manula Mchezaji bora wa Mwaka BMT

17 Mar 2023 By simbasc 363 views
Mlinda mlango, Aishi Manula amechaguliwa mchezaji bora wa mwaka katika hafla ya tuzo zinazotolewa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT). Manula amewapiku walinzi Mohamed Hussein na Shomari Kapombe alioingia ingia nao fainali ya kinyang'anyiro hicho ambao wote wanatoka kwenye kikosi chetu. Tuzo hiyo imepokelewa na Mratibu wa timu, Abbas Ally kutokana na mlinda mlango Aishi kuwa kambini kujiandaa na mchezo wa kesho wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Horoya. Aishi amedaka asilimia kubwa ya mechi zetu pamoja na timu ya Taifa kwa mwaka mzima huku akiwa kwenye ubora mkubwa.
Advertisement
Back to homepage
Share this story