Simba Sports Club
News

Manula arejea rasmi mazoezini

3 Oct 2023

Juni mwaka huu Manula amefanyiwa upasuaji wa nyama za paja nchini Afrika Kusini baada ya kupata majeraha katika mchezo wa robo fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Ihefu FC.

Baada ya takribani miezi minne ya matibabu Manula amepona kabisa na ameanza mazoezi ya uwanjani pamoja na wenzake.

Advertisement

Kwa sasa Manula yupo fiti kuanza kushuka dimbani kutegemea na uhitaji wa benchi la ufundi ingawa anatakiwa kuendana na kasi ya mazoezi na wenzake.

Manula ameukosa mwanzo wa msimu zikiziwemo mechi tatu za Ligi, mechi za Ngao ya Jamii pamoja na mechi mbili za kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Power Dynamos.

Back to homepage
Share this story