Mlinda mlango Aishi Manula leo amefikisha mchezo wa 120 wa ligi kuu tangu alipojiunga nasi msimu wa 2017/18.
Manula amepangwa kuanza katika kikosi chetu kitakachoshuka dimbani muda mfupi ujao kuikabili Geita Gold mchezo utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Tangu alipojiunga nasi Manula amekuwa mlinda mlango namba moja hadi katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Advertisement
Ndani ya miaka minne aliyodumu na kikosi chetu hadi sasa Manula ameibuka kipa bora wa ligi mara zote kutokana na uimara wake.
Kiwango cha Manula kimekuwa kikipanda siku hadi siku kiasi cha kuwavutia makocha wote wanaokuja kiifundisha timu yetu.