Simba Sports Club
News

Manula afanyiwa upasuaji

31 May 2023

Kwa mujibu wa daktari wa klabu Edwin Kagabo aliyeambatana na Manula upasuaji huo wa saa mbili uliofanyika jana Jumanne umekwenda vizuri.

Kwa sasa Manula yuko wodini ambapo ataendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo hadi Ijumaa.

Daktari Kagabo amesema kama kila kitu kitakwenda sawa basi Ijumaa wataruhusiwa kutoka hospitalini na kurejea nyumbani Tanzania.

Advertisement

Daktari Kagabo ameongeza kuwa kwa sasa ni mapema mno kusema Manula atakaa nje kwa muda gani mpaka pale watakapohudhuria kliniki ya mwisho Ijumaaa wiki hii.

Manula alichanika nyama za paja katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Ihefu FC na hivyo klabu imeamua kumtafutia mchezaji huyo matibabu stahiki ili aweze kurejea haraka uwanjani.

Back to homepage
Share this story