Simba Sports Club
News

Mangungu awapokea mashabiki Ndola

15 Sep 2023

Mashabiki hao ambao wamejaza mabasi mawili makubwa wameondoka Dar es Salaam juzi Jumatano saa moja usiku na kufika hapa Ndola leo saa nne asubuhi.

Mangungu amewashukuru mashabiki hao kwa kujitoa kwao hali na mali kuja Zambia kuhakikisha timu inapata ushindi.

Advertisement

"Kwa niaba ya Uongozi wa klabu ya Simba, nawashukuru wote kwa kuja Zambia kuisapoti timu. Uongozi wa Simba unathamini mchango wenu na lengo letu ni kuhakikisha tunapata ushindi," amesema Mangungu

Back to homepage
Share this story