Simba Sports Club
News

Mangungu aongoza Wanasimba kumuaga Dk. Gembe

4 Sep 2022

Mangungu ameongozana na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na wachezaji nyumabani kwa marehemu Mbweni kabla ya kusafirishwa kuelekra Korogwe, Tanga kwa mazishi.

Baada ya kudumu kama daktari wa timu wa klabu yetu kwa takribani miaka 10 Gembe alipewa majukumu mengine ya kuwa daktari wa timu ya vijana nafasi aliyodumu nayo mpaka anakutwa na mauti.

Advertisement

Mwili wa marehemu Dk. Gembe utazikwa kesho Jumatatu nyumbani kwao Manundu, mjini Korogwe.

Back to homepage
Share this story