Simba Sports Club
News

Maneno ya Robertinho tukiifuata Vipers, amtaja Kanoute

23 Feb 2023

Robertinho amesema anafahamu mchezo utakuwa mgumu na tunaenda kukutana na ushindani mkubwa lakini tumejipanga kwa kila hali.

Robertinho ameongeza kuwa katika mchezo huo tunahitaji kupata ushindi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele na wachezaji wameandaliwa vizuri juu ya hilo.

"Tumepata muda wa maandalizi wa kutosha kuelekea mchezo dhidi ya Vipers. Tunajua utakuwa mgumu hasa kwa kuwa tunaenda ugenini lakini tumejiandaa kwa hilo.

Advertisement

"Nafurahi kurejea kwa mchezaji Sadio Kanoute ambaye alikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Raja Casablanca kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

"Kanoute ni mchezaji mzuri wa kikosi cha kwanza na tunaamini atakuwa msaada katika mchezo dhidi ya Vipers," amesema Robertinho.

Back to homepage
Share this story