Simba Sports Club
News

Mambo sita ya kufahamu kuelekea mchezo wetu wa leo dhidi ya Al Ahly

5 Apr 2024

Tumekueka mambo sita kufahamu kuelekea mchezo wetu wa pili wa robo fainali

1. Ni mara ya kwanza kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

2. Sio kitu kigeni kwa Simba kupata matokeo chanya katika ardhi ya Misri. Tuliwahi kuwatoa Zamalek mwaka 2003.

3. Hii mara ya nne kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni ya pili mfululizo.

Tumecheza miaka ya (2019, 2021, 2023).

4. Fabrice Ngoma ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi dhidi ya Al Ahly.

- Amecheza mechi 14 dhidi ya Al Ahly akiwa na timu nne tofauti ambazo ni:

Advertisement

AS Vita mechi 6

Raja Casablanca mechi 4

Al Hilal mechi 1

Simba mechi 3

5. Wachezaji wanne, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr', Clatous Chama, Mzamiru Yassin na Ally ndio wachezaji waliocheza robo fainali nne tulizocheza ndani ya miaka mitano.

6. Misri ndio nchi inayoongoza kwa timu zake kukutana na Simba kwenye michuano ya Afrika.

Tumewahi kukutana na timu na Ismailia, Haras El Hodoud, Zamalek na Al Ahly.

Back to homepage
Share this story