Simba Sports Club
News

Mambo matano ya kuyafahamu kuelekea mchezo wetu dhidi ya RS Berkane

17 May 2025

1. Tunakutana kwa mara ya pili kwenye michuano hii. Tulikutana mwaka 2022 katika hatua ya makundi.

2. Kila timu ilishinda mechi yake yake ya nyumbani. (27/02/2021 tulipoteza kwa mabao 2-0 ugenini, Machi 13 tuliibuka na ushindi wa bao moja katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

3. Ni wachezaji watano pekee ndio walikuwepo kwenye kikosi chetu kilichocheza mechi dhidi ya Berkane. Nyota hao ni Aishi Manula, Ally Salim, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' na Mzamiru Yassin.

Advertisement

4. Hii ni fainali yetu ya pili ya michuano hii baada ya kupita miaka 32. Mara ya mwisho kucheza ilikuwa mwaka 1993.

5. Kwenye hatua ya makundi wote tuliibuka vinara wa kundi. Tuliongoza kundi A tukiwa na alama 13 wakati Berkane waliongoza kundi B wakiwa na alama 16.

Back to homepage
Share this story