Mambo matano ya kufahamu kuelekea mchezo dhidi ya ES Tunis
1. Hii ni mara ya Kwanza kucheza ES Tunis.
2. Tunaenda kucheza mechi za Afrika nchini Tunisia kwa mara ya pili Mwaka jana tulicheza Kombe la Shirikisho dhidi ya CS Sfaxien.
Advertisement
3. Mchezo wa mwisho kucheza katika ardhi ya Tunisia tulipata ushindi wa bao moja ambalo lilifungwa na kiungo mshambuliaji, Jean Charles Ahoua.
4. Ni wachezaji watatu tu ambao wapo kikosini na walikuwepo tulipokuja Tunisia mwaka jana. Nyota hao ni nahodha, Shomari Kapombe, David Kameta na mlinda mlango, Hussein Abel.
5. Kocha Mkuu Steve Barker atakuwa anasimamia mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa. Msimu uliopita aliiongoza Stellenbosch lakini ilikuwa Kombe la Shirikisho Afrika.