Simba Sports Club
News

Mambo matano usiyoyajua kuhusu mchezo wetu dhidi ya Wydad

28 Apr 2023

1. Ni mara ya Kwanza kwetu kucheza katika Uwanja wa Mohamed wa V na timu mbili kubwa za Morocco ndani ya msimu mmoja.

2. Tunahitaji Sare ya aina yoyote au ushindi kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

3. Ni wachezaji sita tu waliopo kwenye kikosi cha sasa ambao waliocheza robo fainali ya kwanza ya Simba dhidi ya TP Mazembe ambao ni Aishi Manula, Mohammed Husein, Erasto Nyoni, Mzamiru Yassin, John Bocco na Clatous Chama.

Advertisement

4. Nyota watatu Ally Salim, Saido Ntibazonkiza na Jean Baleke ni mechi yao ya kwanza ugenini ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa Simba.

5. Ni mara ya kwanza mlinda mlango Aishi Manula kukosekana katika mchezo wa ugenini wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa tangu ajiunge nasi Juni, 2017.

Back to homepage
Share this story