Simba Sports Club
News

Mambo matano usiyoyajua kuhusu mchezo wa Horoya vs Simba

10 Feb 2023

Kuna mambo ambayo huenda huyafahamu kuhusu mchezo huo, hapa tumekuwekea matano tu...

1. Horoya vs Simba hazijawai kukutana hata mara moja katika historia ya soka.

2. Hii ni mara ya kwanza Simba kufika Guinea na kucheza mechi ya kimashindano.

3. Sadio Kanoute na Pape Sakho ndiyo wachezaji wetu wanaotajwa sana na vyombo vya habari nchini hapa ndiyo wachezaji maarufu.

Advertisement

Kanoute amekuja mara kadhaa na Timu ya Taifa ya Mali wakati Sakho anatajwa kwa kufunga bao bora la mashindano msimu uliopita.

4. Uwanja wa Septemba 28 ndiyo Uwanja wa Horoya ambao umefungiwa na CAF kwa kuwa haujakidhi vigezo.

Mchezo wetu utapigwa katika Uwanja wa timu ya Taifa ya Guinea unaoitwa Jenerali Lansana Conte.

5. Mashabiki 500 pekee ndiyo wameruhisiwa na CAF kushuhudia mchezo wa kesho.

Back to homepage
Share this story