Simba Sports Club
News

Mambo matano usiyoyajua kuelekea Ngao ya Jamii

10 Aug 2023

Tumekuandalia mambo matano usiyoyajua ndani ya kikosi chetu kuelekea mashindano haya mafupi ambayo yatakamilika Agosti 13.

1. Mabadiliko ya Mfumo wa Mashindano

Kanuni za Ngao ya Jamii msimu huu imebadilika na itashirikisha timu nne ambazo zimemaliza nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi msimu uliopita.

2. Ngao ya Jamii ya kwanza ya Robertinho

Mchezo wa leo utakuwa wa kwanza wa Ngao ya Jamii kwa kocha mkuu, Roberto Oliviera 'Robertinho' pamoja na benchi lake ufundi.

Robertinho amejiunga nasi msimu uliopita lakini wakati anakuja tulikuwa tayari timecheza mchezo wa Ngao ya Jamii.

3. Zimbwe Jr, Kapombe, Bocco vinara Ngao ya Jamii

Wachezaji watatu Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' Shomari Kapombe na nahodha John Bocco wanaongoza kwa kucheza mechi nyingi za Ngao ya Jamii ndani ya kikosi chetu.

Advertisement

Kila mmoja amecheza mechi sita na leo itakuwa ya saba. Katika mechi hizo tumeshinda nne nakupoteza mbili tangu mwaka 2017.

4. Manula anakosa Ngao ya tatu mfululizo

Mlinda mlango namba moja Aishi Manula atakosa mechi za Ngao ya Jamii na hii itakuwa mara ya tatu mfululizo.

Mara zote mbili zilizopita mechi ya Ngao ya Jamii amedaka mlinda mlango Beno Kakolanya.

5. Nyota nane kushiriki kwa mara ya kwanza Ngao ya Jamii

Wachezaji tisa wapya tuliowasajili msimu huu watashiriki mchezo wa Ngao ya Jamii kwa mara ya kwanza.

Nyota hao ni Hussein Abeli, Hussein Kazi, Abdallah Hamis, Will Essomba Onana, Che Fondoh Malone, Aubin Kramo, David Kameta, Shaban Chilunda na Fabrice Ngoma.

Luis Miquissone tumemsajili dirisha hili lakini amewahi kushiriki Ngao ya Jamii alipokuja mara ya kwanza.

Back to homepage
Share this story