Simba Sports Club
News

Mambo matano kuhusu mchezo wetu dhidi ya Al Masry

2 Apr 2025

Tumekuandalia mambo matano ya kuyafahamu kuelekea kwenye mchezo wa leo.

1. Ni mara ya pili kukutana katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mwaka 2018 tukikutana hatua ya awali lakini sasa tunakutana Robo Fainali.

2. Mechi ya Simba dhidi ya Al Masry haijawahi kutoa mshindi ndani ya dakika 90. Mwaka 2018 tulitoka sare ya 2-2 nyumbani na ugenini 0-0.

Advertisement

3. Ni wachezaji wanne tu ambao wapo kikosini kwa sasa na walikuwepo tulivyocheza na Al Masry mwaka 2018. Nyota hao ni Aishi Manula, Shomari Kapombe Mohamed Hussein na Mzamiru Yassin.

4. Mchezo huu utapigwa katika Uwanja wa Suez Canal lakini ule uliopita ulichezwa Uwanja wa Borg El Arab.

5. Hii ni robo fainali ya sita kwa Simba kwenye michuano ya Afrika (Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho) katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

Back to homepage
Share this story