Simba Sports Club
News

Mambo matano kuelekea mchezo wetu dhidi ya Stade Malien

30 Nov 2025

Tumekuekea mambo matano kuelekea mchezo huo

1. Ni mara ya kwanza Simba kucheza mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika katika nchi ya Mali

2. Hakuna mchezaji yeyote ambaye anatokea nchi ya Mali katika kikosi chetu

Advertisement

3. Shomari Kapombe ndiye mchezaji pekee aliyopo kwenye kikosi tangu tulipoanza kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika mwaka 2017 na ameambatana na timu akiwa nahodha.

4. Tanzania Na Mali tunatofautiana saa tatu. Mchezo wetu wa leo utapigwa saa 10 kwa saa za Mali ambapo Tanzania itakuwa saa moja usiku.

5. Mchezo wa leo utachezeshwa na mwamuzi, Andofetra Manda kutoka nchini Madagascar.

Back to homepage
Share this story