Simba Sports Club
News

Mambo Matano Kuelekea mchezo wetu dhidi ya Gaborone United

20 Sep 2025

1. Ni mara ya tatu Simba inacheza mechi za kimataifa nchini Botswana katika kipindi cha miaka mitano, na ni mara ya pili inacheza mechi katika mji wa Fransictown na ni mara ya pili inacheza katika Uwanja wa Obed Itani Chilume.

2. Simba haijawahi kupoteza mchezo wowote chini Botswana. Mara mbili tumecheza dhidi ya Jwaneng Galaxy ambapo mchezo wa kwanza tulishinda 2-0, na mechi ya pili ilikuwa sare ya 0-0.

3. Simba haijawahi kuruhusu bao hata moja nchini Botswana

Advertisement

4. Shomari Kapombe na Muzammil Yassin ndio wachezaji pekee waliocheza mara zote mbili dhidi ya Jwaneng Galaxy na leo wapo kikosini tayari kuivaa Gaborone.

5. Fadlu Davids anakuwa kocha watatu kuileta Simba nchini Botswana baada ya Didier Gomez mwaka 2021 na Abdelhak Benchika mwaka 2023.

Back to homepage
Share this story