Simba Sports Club
News

Mambo 10 kuelekea mchezo wetu dhidi ya Vipers

24 Feb 2023

2. Timu hazijawahi kukutana katika mchezo wowote hata mechi ya kirafiki.

3. Kocha Roberto Oliviera 'Robertinho' amezifundisha timu zote kwa nyakati tofauti na ndiye aliiwezesha Vipers kuingia hatua ya makundi. Kwa sasa ndiye kocha wetu mkuu.

4. Timu zote zinatoka kwenye majiji makubwa, Vipers inatoka Kampala, Simba Dar es Salaam.

5. Vipers ina alama moja kwenye Kundi C, sisi bado hatujapata.

6. Juuko Murshid ndiye mchezaji pekee aliyecheza timu zote mbili. Alikuwa mchezaji wetu kuanzia 2014/2019 sasa anaitumikia Vipers.

Advertisement

7. Tumecheza wote siku moja mechi za ligi Jumatano wao wamecheza na Wakiso Giants wakatoka sare ya bila kufungana sisi tumecheza na Azam FC tukatoka 1-1.

8. Vipers hawajafunga bao lolote kwenye hatua ya makundi mpaka sasa kama sisi.

9. Vipers wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi nchini Uganda.

10. Vipers wanatumia Uwanja wa St. Mary's uliopo mji wa Katende wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 15,000.

Back to homepage
Share this story