Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez amesema awamu ya kwanza ya usaili itawahusu makocha wanne kati ya 10 waliobaki kwenye orodha ya mwisho.
Zaidi ya makocha 100 kutoka sehemu mbalimbali duniani waliomba kazi ambapo katika mchujo wa awali walibaki 40 na wa pili wamebaki 10 ambao kati ya hao wanne ndiyo wanafanyiwa usaili.
"Baada ya kupokea wasifu wa makocha kutoka sehemu mbalimbali duniani sasa tupo kwenye hatua ya pili ambapo wanne tunawafanyia usajili na mmoja atakayekidhi vigezo tutampa kazi," amesema Barbara.
Barbara amebainisha kuwa tunatarajia usaili utamalizika ndani ya siku chache zijazo hadi kufika katikati ya mwezi huu kocha mpya atakuwa ameshapatikana ili ashuhudie mechi zilizobaki na kutoa mapendekezo ya usajili wa msimu ujao.