Simba Sports Club
News

Makocha 100 watuma CV

7 Jun 2022

Tayari kikao cha kwanza cha mchujo kimeketi na kuangalia wasifu wao na ambapo yamekatwa na kubaki majina 40 ya ambao wataingia kwenye hatua ya pili.

Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez amesema idadi kubwa ya makocha waliotuma wasifu wao ni kutoka barani Ulaya na Amerika ya Kusini

Barbara ameongeza kuwa mchakato wa kumpata kocha mpya utakamilika ndani ya wiki mbili na atatua nchini kuangalia mechi za mwisho za ligi ili kuona mapungufu na kusimamia usajili.

Advertisement

Barbara amesema tunampa nafasi kocha anayejua vizuri soka la Afrika ambapo akiwa mzawa itakuwa vizuri huku aliyetuma ni mmoja na hana vigezo jambo ambalo linachelewesha mchakato.

"Tumepokea wasifu wa makocha zaidi ya 100 kutoka sehemu mbalimbali duniani ambao wengi wao ni kutoka barani Ulaya na Amerika Kusini. Mchakato wa mchujo unaendelea na tunategemea utakamilika ndani ya wiki mbili zijazo.

"Tunahitaji kocha anayejua vizuri soka la Afrika pia tungefurahi kupata kocha ambaye ni mzawa wa bara hili lakini mpaka sasa bado hawajatuma wasifu na aliyetuma ni mmoja na vigezo vyake havitoshi," amesema Barbara.

Back to homepage
Share this story