Simba Sports Club
News

Mainstream, Nexus watengenezaji wa kadi za wanachama

10 Feb 2026

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Crescentius Magori amesema mchakato wa kupata kadi mpya za wanachama umechukua muda mrefu kwa sababu tulikuwa tunatafuta Kampuni bora kwa ajili ya utengenezaji na ndio tumeipata.

"Leo tumekusanyika hapa kwa jambo la muda mrefu ambalo limesubiriwa sana. Tulikuwa tunatafuta kampuni ya uhakika kutengeneza kadi za Simba, kadi ambazo zinafanana na timu kubwa kabisa Afrika."

"Bodi ya Wakurugenzi inapenda kuitangaza kampuni ya Mainstream kuwa ndio itatengeneza kadi za mfumo wa kisasa na imeichagua kampuni ya Nexus kutoa kadi hizi za wanachama ambazo zitakuwa zitakuwa aina ya VISA.”

"Hii inakwenda kuwa Visa card pamoja na kukutambua kwamba ni mwanachama wa Simba lakini pia unaweza kuweka pesa, ukafanya malipo na miamala," amesema Magori.

Advertisement

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Murtaza Mangungu ameweka wazi kuwa kadi hizo zitaanza kutolewa Machi 27 mwaka huu

"Tumeingia mkataba na wenzetu Mainstream Group na Nexus Pesa, utoaji wa kadi utafata katiba ya Simba kuanzia ngazi ya matawi hadi makao makuu ya klabu."

"Tumepanga kuanza kutoa kadi tarehe 27 Machi mwaka huu, tunafanya hivyo sababu kuna mambo mengi na Taasisi nyingi zinahusika katika maandalizi ya utoaji wa hizo kadi," amesema Mangungu.

Back to homepage
Share this story