Simba Sports Club
News

Magori, Nkwabi wamtembelea Nangu Kilimanjaro

13 Mar 2026

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Crescentius Magori akiongozana na Mjumbe wa Bodi, Swedi Mkwabi, Mjumbe wa Kamati ya Mashindano, Habibu Nasser na Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally hii leo wamemtembelea Mchezaji Wilson Nangu ambae anauguza majeraha nyumbani kwao Boma N’gombe, Kilimanjaro.

Nangu alipata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Esparance Du Tunis uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Februari Mosi na hivyo kumuweka nje hadi mwisho wa msimu.

Tayari Nangu ameshafanyiwa upasuaji nchini Afrika kusini na sasa anaendelea kujiuguza nyumbani kwao Boma N’gombe, Kilimanjaro.

Akizunguma katika ziara hiyo Magori amesema ni jukumu la viongozi wa juu kuwajulia hali wachezaji wao hasa wakiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo maradhi.

Advertisement

"Jukumu la Viongozi ni kuhakikisha ustawi wa wachezaji wake, sio tu kulipa mishahara bali pia kuwa karibu nao wanapopata changamoto ya kiafya kama ilivyo kwa Nangu. Sote tunafahamu uwezo wa Nangu na tunamuombea apone haraka ili arejee kikosini," amesema Magori.

Kwa upande wake, Nangu amesema amefurahi viongozi wake kumtembelea nyumbani ambapo imekuwa faraja kwakwe huku akisema kwa sasa anaendelea vema na hasikii maumivu mguuni.

"Nimefarijika kuwaona Viongozi wangu mmekuja nyumbani kuniona kuhusu afya yangu kwa sasa naendelea vizuri muda wowote kuanzia sasa nitakwenda kutoa P.O.P ikiwa ni hatua kubwa ya kuendelea kupona," amesema Nangu.

Nangu anatarajiwa kukaa nje hadi mwisho wa msimu na atarajea rasmi uwanjani Julai katika maandalizi ya msimu mpya 2026/2027 (Pre Season).

Back to homepage
Share this story