Simba Sports Club
News

Maandalizi ya Mchezo dhidi ya Singida FG yanaendelea vizuri

9 Jan 2024

Matola amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na hakuna yoyote ambaye tutamkosa kutokana na majeraha au kutumikia adhabu ya kadi.

Matola ameongeza kuwa itakuwa mechi ngumu hasa ukilinganisha Singida tumetoka kuifunga wiki iliyopita katika mchezo wa hatua ya makundi.

"Kikosi kipo tayari kwa mchezo, wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo wa kesho. Tunaushukuru kuwa hakuna mchezaji ambaye tutamkosa kutokana nakuwa majeruhi au kutumikia adhabu," amesema Matola.

Advertisement

Aidha Matola ameweka wazi kuwa winga mpya Ladack Chasambi anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Singida kesho kwakuwa nae atakuwepo kwenye mazoezi ya mwisho ya maandalizi leo jioni.

"Ladack ni mchezaji mpya na yupo na kikosi hapa Zanzibar, tunategemea atakuwa sehemu ya kikosi katika mchezo wa kesho," amesema Matola.

Back to homepage
Share this story