Simba Sports Club
News

Maandalizi ya Geita Kesho yamekamilika

17 Dec 2022

Mgunda amesema kikosi kipo katika hali nzuri wachezaji wote 24 ambao wamesafiri wapo kamili kupambana kuhakikisha pointi tatu zinapatikana.

Mgunda ameongeza kuwa tunaiheshimu Geita na tunategemea kupata upinzani mkubwa lakini tumejidhatiti kuhakikisha tunashinda.

"Maandalizi yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri, tunaiheshimu Geita na tunategemea kupata ushindani mkubwa kesho lakini tupo tayari kuwakabili," amesema Mgunda.

Advertisement

Kwa upande wake Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema wachezaji wapo tayari kufuata maelekezo ya benchi la ufundi ili kuhakikisha pointi tatu zinapatikana.

"Sisi kama wachezaji tupo tayari kufuata maelekezo tutakayopewa na walimu wetu ili kushinda. Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Geita na tunawaheshimu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda," amesema Zimbwe Jr.

Back to homepage
Share this story