Simba Sports Club
News

Maafisa wa CAF watua kufanya ukaguzi wa Super Leagur

16 Feb 2023

Sisi ni miongoni mwa timu nane barani Afrika ambazo zimechaguliwa kushiriki michuano hiyo mipya ambayo itakuwa ndio mara ya kwanza kufanyika.

Maafisa hao watakagua maeneo yote muhimu yanayohitajika kwa ajili ya michuano hiyo kama viwanja vya mazoezi, Uwanja wa mchezo pamoja na Hoteli.

Advertisement

Uongozi wa klabu umewapokea Maafisa hao tangu walipofika nakuwapa ushirikiano wote wanao uhitaji ili kukamilisha kazi yao kwa haraka kwa muda unaotakiwa.

Baada ya zoezi la ukaguzi kukamilika kwa timu zote shiriki Kamati zitakutana kwa ajili ya kufanya majumuisho na kupanga utaratibu wa mashindano jinsi yatakavyokuwa, muda pamoja na ratiba.

Back to homepage
Share this story