Lukula amesema wachezaji wamecheza vizuri na wamepambana kuanzia mwanzo hadi mwisho jambo ambalo limetufanya kufanikiwa kufikia hatua hiyo.
Lukula ameongeza kuwa baada ya kuona timu inapoteza nafasi kipindi cha kwanza tulivyokwenda mapumziko alifanya mabadiliko ya kuongeza washambuliaji na kuifanya timu kutulia na kusababisha timu kupata ushindi.
Advertisement
"Nawapongeza wachezaji wangu wamecheza vizuri, wamepambana kwa ajili ya timu, haikuwa rahisi kufika hatua hii. Ilikuwa mechi ngumu lakini tunashukuru tumevuka.
"Tulicheza vizuri na kumiliki sehemu kubwa ya mchezo, kipindi cha kwanza tulipoteza nafasi nyingi lakini cha pili niliwatuliza na kuwaambia wasiwe na presha mabao yatakuja na tukafanikiwa," amesema Lukula.