Mchezo huu ni wa pili wa kirafiki baada ya ule tuliocheza dhidi ya Al Qanah ambao tuliibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Tulivyomaliza wiki ya kwanza ya mazoezi tulivyofika nchini Misri tulicheza mechi ya wenyewe kwa wenyewe ambapo wachezaji wetu waligawanywa kwenye makundi mawili.
Advertisement
Mchezo wa leo utaendelea kumpa nafasi kocha Fadlu Davids na wasaidizi wake kuona wachezaji wameyashika mafunzo kwa kiasi gani.
Tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Telecom na tunaamini kitakuwa kipimo kizuri kwetu.