Simba Sports Club
News

Leo tunacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Batman A.S

30 Jul 2023

Mchezo wa leo utakuwa watatu wa kirafiki tangu tufike Uturuki, benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliviera 'Robertinho' litazidi kuona ubora na mapungufu ya timu ilipofikia mpaka sasa.

Kocha Robertinho ameweka wazi kufurahishwa na hali ya kikosi ilipofikia kuanzia utimamu wa mwili mpaka mbinu za uwanjani.

Advertisement

Jambo jema ni kwamba mpaka sasa hakuna mchezaji yoyote aliyepata majeraha ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa leo.

Back to homepage
Share this story