Simba Sports Club
News

Leo tunaanza mchezo wa kirafiki

24 Jul 2023 By simbasc 354 views
Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitacheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Zira FC 'The Eagles' utakaofanyika katika Uwanja wa Bolu hapa Uturuki. Zira ni timu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Azerbaijan na ipo Uturuki kwa ajili ya kambi ya maandalizi kujiandaa na msimu mpya wa mashindano 2023/24 kama ilivyo kwetu. Hii ni mechi ya kwanza ya kirafiki tangu tufike hapa Uturuki na italipa mwanga benchi la ufundi kuona jinsi gani wachezaji wanaelewa mafunzo wanayowapa.
Advertisement
Back to homepage
Share this story