Simba Sports Club
News

Leo tuna mechi mbili za kirafiki dhidi ya Turan PFK

27 Jul 2023

Turan Tovuz PFK ni timu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Azerbaijan na benchi la ufundi linaamini itatupa kipimo kizuri kwa wachezaji wetu.

Lengo la kucheza mechi mbili na timu moja ni kuwapa nafasi wachezaji wote kushiriki ili kuona ni kiasi gani wameelewa pamoja na utimamu wao.

Advertisement

Mchezo wa kwanza utachezwa saa 5:00 Asubuhi ambapo wataocheza hawatapangwa tena kwenye mechi ya pili ilitakayopigwa saa 12:00 jioni.

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera 'Robertinho' na wasaidizi wake wanataka kukiona kikosi chetu kwa mapana ili kujua walipofikia kabla ya kuanza mashindano.

Back to homepage
Share this story