Simba Sports Club
News

Lakred aanza mazoezi rasmi

15 Aug 2023

Lakred tumemsajili wiki iliyopita kutoka kwa Mabingwa wa Morocco, FAR Rabat tayari amejiunga na kikosi na yupo mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa keshokutwa Alhamisi.

Lakred amefanya mazoezi moja kwa moja na walinda milango wenzake Ally Salim, Hussein Abeli na Ahmed Feruz chini ya kocha Daniel Cadena.

Advertisement

Pamoja nakuwa ni siku yake ya kwanza mazoezini akiwa na kikosi chetu Lakred ameonyesha uwezo mkubwa na kuyafuata vema maelekezo aliyokuwa akipewa na kocha Cadena.

Tunaamini uwezo wa Lakred utazidi kuimarisha kikosi chetu na kocha mkuu Roberto Oliviera 'Robertinho' atakuwa na wigo mpana wa uchaguzi wa timu kulingana na mchezo husika.

Back to homepage
Share this story