Kyombo amesema amezoea mazingira haraka kutokana na ushirikiano anaopata ndani na nje ya uwanja pamoja na benchi la ufundi chini ya Kocha Zoran Maki.
Kuhusu kambi inayoendelea hapa Misri, Kyombo amesema mazoezi yanaendelea vizuri na kila mchezaji anajituma ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi.
Kyombo amekiri baada ya kupangwa kwenye kikosi cha kwanza kilichocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ismailia wiki iliyopita alikuwa na hofu lakini baadaye alizoea na kufanya vizuri.
"Kwa kweli nimefurahi jinsi wachezaji wenzangu walivyonipokea, wamenipa ushirikiano mkubwa. Simba ni timu kubwa na jinsi inavyoonekana nje ni tofauti tunaishi kwa upendo mkubwa.
"Maandalizi tunayofanya ni makubwa na nina imani tutakaporudi nyumbani tutakuwa bora na tunaweza kutetea ubingwa wetu," amesema Kyombo.