Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu alichodumu nasi akitokea klabu ya Geita Gold Fc, Ntibazonkiza amekuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza akiwa mfungaji bora wa timu yetu katika misimu yote miwili na klabu inathamini mchango wake .
Msimu wa 2022/23 Saido Ntibazonkiza alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kufunga mabao 17 huku pia akiibuka kiungo bora wa msimu.
Licha ya kucheza kwa muda mfupi Ntibazonkiza ameacha alama ndani ya kikosi kutokana utumishi uliotukuka ndani na nje ya uwanja.
Advertisement
Uongozi wa klabu unamtakia kheri Ntibazonkiza katika maisha yake mapya ya soka nje ya timu ya Simba.
Kuachana na Saido Ntibanzokiza ni hatua za klabu yetu kuendelea kufanya maboresho makubwa ya kikosi kwa ajili ya msimu ujao