Kanoute alijiunga nasi msimu wa 2021/22 kutoka klabu ya Al Ahly Benghazi ya Libya kwa miaka mitatu ambayo tumekuwa na uhusiano mzuri baina yetu.
Mkataba wa Kanoute umemalizika rasmi na baada ya mazungumzo ya pande mbili tumekubalina kutokuwa pamoja.
Advertisement
Kanoute ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wakijitoa katika muda wote wa mchezo na kuhakikisha anaisaidia timu kupata ushindi.
Simba inathamini mchango mkubwa aliotoa Kanoute katika kipindi chote cha miaka mitatu tulichodumu nae na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya nje ya kikosi chetu.