Simba Sports Club
News

Kwaheri Pa Omar Jobe

16 Jul 2024

Jobe (25) raia wa Gambia amejiunga nasi katika dirisha la usajili la mwezi Januari akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya Zhenis inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kazakhstan.

Jobe ni mmoja ya washambuliaji bora na mwenye uwezo mkubwa lakini ameshindwa kuendana na kasi ya timu na malengo ya klabu.

Katika kipindi chote alichokuwa nasi Jobe alikuwa mchezaji msikivu mwenye nidhamu ya hali ya juu na alikuwa anajituma mazoezini na uwanjani.

Advertisement

Kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/25 tumefanya marekebisho makubwa ya kikosi na malengo yetu ni kurejesha makali tuliyokuwa nayo miaka minne iliyopita.

Simba inamtakia kheri Jobe katika maisha mapya ya soka nje ya Simba na siku zote tutaendelea kuthamini mchango wake ndani ya kikosi chetu.

Back to homepage
Share this story