Simba Sports Club
News

Kwaheri Nelson Okwa

21 Jun 2023

Okwa alijiunga na kikosi chetu Julai, 2022 kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Rivers United ya nchini Nigeria.

Novemba mwaka jana tulimtoa kwa mkopo katika klabu ya Ihefu FC alipocheza kwa miezi sita mpaka msimu wa ligi 2022/23 unamalizika.

Advertisement

Kutokana na benchi la ufundi kuona hatakuwa kwenye mpango wake kuelekea msimu mpya wa ligi Uongozi wa klabu umemuita Okwa na kukaa chini na kukubaliana kuachana.

Okwa anakuwa mchezaji wa nne kuachana nae kuelekea kusuka kikosi chetu kwa ajili ya msimu ujao wa ligi 2023/24 baada ya Augustine Okrah, Mohamed Ouattara na Victor Akpan.

Back to homepage
Share this story