Violeth amejiunga nasi msimu wa 2018 akitokea Kigoma Sisters ambapo kabla ya hapo amepitia timu ya Evergreen Queens.
Katika kipindi cha miaka miaka saba amekuwa mchezaji tegemezi pamoja na kiongozi wa timu uwanjani.
Violeth ameiongoza Simba Queens kushinda mataji ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) katika misimu ya:
2019/2020
Advertisement
2020/2021
2021/2022
2023/2024
Akiwa ndani ya kikosi cha Simba Queens Violeth ameshiriki michuano ya Cecafa mara tatu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo alifika hatua ya nusu fainali.