Mkude ambaye alitoka kwenye kikosi chetu cha vijana na na kupandishwa katika timu ya wakubwa mwaka 2011 ambapo amedumu na timu bila kuhama mpaka leo.
Mpaka sasa Mkude anashirikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyedumu na kikosi chetu kwa muda mrefu zaidi ya wachezaji wote waliopo sasa baada ya kukaa kwa miaka 12
Mkude amewahi kuwa nahodha wa kikosi chetu na ametwaa mataji matano ya Ligi Kuu katika miaka ya:
2012
2018
2019
2020
2021.
Mkude pia ameshinda mataji matatu ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) katika miaka ya:
2017
2020
2021.
Pia amechukua mataji ya Mapinduzi mara mbili miaka ya:
2015
2022
Mkude ameshinda taji la Ngao ya Jamii mara nne kwa muda wote wa miaka 13 aliyodumu na kikosi chetu.
Uongozi wa klabu unamshukuru Mkude kwa utumishi wake uliotukuka kwa muda wote aliokuwa nasi na kumtakia kheri katika maisha mapya nje ya kikosi chetu.