Simba Sports Club
News

Kwaheri Mo Ouattara

20 Jun 2023

Ouattara tumemsajili Julai 2022 kutoka Al Hilal ya Sudan kwa mkataba wa mwaka mmoja huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwingine mmoja.

Tulikuwa na matarajio makubwa na Ouattara kutokana na uwezo aliokuwa nao kabla ya kujiunga nasi lakini hali ilikuwa tofauti huku majeraha nayo yakichangia sehemu kubwa.

Baada ya msimu kumalizika benchi la ufundi limeona Ouattara hayupo sehemu ya mipango yao hivyo Uongozi umeamua kumalizana nae.

Advertisement

Kuachana na Ouattara ni sehemu ya marekebisho makubwa ya kikosi ambayo tunayafanya kuelekea msimu mpya wa ligi 2023/24.

Ouattara anakuwa mchezaji wa tatu kuachana nae baada ya Augustine Okrah na Victor Akpan ikiwa ni sehemu ya kusuka kikosi kipya.

Back to homepage
Share this story