Simba Sports Club
News

Kwaheri Luis Miqussone

19 Jun 2024

Miquissone alisaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezeka kama kiwango chake kitaridhisha lakini kutokana kiwango duni alichoonesha klabu imeamua kutomuongezea mkataba mwingine.

Miquissone alijiunga nasi kwa mara ya kwanza Januari 2020 akitokea UD Songo ya Msumbiji ambako alikuwa anacheza kwa mkopo kutoka Mamelodi Sundowns na katika kipindi hicho alionyesha uwezo mkubwa na kuibuka kipenzi cha Wanasimba.

Julai 22 mwaka jana Miquissone alirejea tena Simba kutoka Al Ahly ambapo tulimuuza lakini hata hivyo makali yake hayakuweza kuwa kama ya awali hivyo Uongozi umeamua kutomuongezea mkataba.

Tangu amejiunga nasi msimu huu amecheza mechi 19 za ligi kuu ya NBC akitoka assist tatu, huku akifunga bao moja pekee katika mashindano ya Mapinduzi.

Advertisement

Uongozi umedhamiria kufanya maboresho makubwa ya kikosi kuelekea msimu ujao wa Ligi na Miquissone hayupo kwenye mipango ya timu.

Hata hivyo Simba inabaki kuwa familia kwa Miqussone na muda wowote anakaribishwa tena kutokana na mambo makubwa aliyotufanyia.

Tunamtakia kila la kheri Miquissone katika maisha mapya ya soka nje ya kikosi cha Simba.

Back to homepage
Share this story