Simba Sports Club
News

Kwaheri Lionel Ateba

24 Aug 2025

Alteba (25) alijiunga na timu yetu Agosti mwaka jana akitokea USM Algiers ya Algeria kwa mkataba wa miaka miwili lakini baada ya kupokea ofa kutoka kwa Al Shorta tumekubali kufanya biashara.

Ateba alikuwepo kwenye kikosi chetu kilichopo Misri kinachoendelea na maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2025/2016.

Tayari Ateba raia wa Cameroon ameruhusiwa kuondoka kambini kwenda kujiunga na Al Shorta ili kuendelea na maandalizi akiwa na timu yake mpya.

Advertisement

Simba tumekuwa utaratibu mzuri wa kuwaachia wachezaji wetu kwenda kujiunga na timu nyingine hasa linapokuja suala zima la maslahi kwa pande zote mbili za mchezaji pamoja na Klabu.

Uongozi wa klabu ya Simba unamtakia Kheri Ateba kwenye maisha yake mapya ya soka.

Back to homepage
Share this story