Simba Sports Club
News

Kwaheri 'Lejendari' John Bocco

17 Jun 2024

Nahodha Bocco hatakuwa sehemu ya kikosi kama ilivyozoeleka lakini bado yupo ndani ya klabu ambapo sasa atahudumu kama kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17.

Bocco alijiunga nasi msimu wa 2017/18 akitokea Azam FC na kutoka hapo amekuwa muhimili wa timu ndani na nje ya uwanja.

Bocco amekuwa msaada mkubwa kwa wachezaji vijana pamoja na wale wageni waliokuwa wakija kikosini na alikuwa kiunganishi bora kati ya Uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.

Advertisement

Katika kipindi cha miaka saba Bocco aliyodumu kikosini ameiongoza timu kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu mfululizo pamoja na Kombe la FA. Pia mataji mengine yakiwemo Kombe la Mapinduzi.

Kutokana na umuhimu wa Bocco Uongozi umeona atakuwa mtu muhimu katika kuwapika na kuzalisha vijana wengine ambao watakuwa msaada kwa Klabu katika siku za baadae.

Bocco anakuwa nahodha wa tatu baada ya Nico Nyagawa na Mussa Mgosi kuwa sehemu ya benchi la timu za Vijana.

Back to homepage
Share this story