Simba Sports Club
News

Kwaheri kiraka Erasto Nyoni

22 Jun 2023

Erasto ni miongoni mwa wachezaji wazawa wenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani kwa weredi mkubwa huku nidhamu yake ikiwa ni ya kuigwa.

Erasto alijiunga nasi Julai 2, 2017 akitokea Azam FC ambapo kwa miaka sita aliyodumu katika kikosi chetu amekuwa muhimili mkubwa.

Erasto ameshiriki kikamilifu katika kikosi chetu kilichochukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania mara nne mfululizo 2018, 2019, 2020 na 2021.

Advertisement

Pamoja na kubadilisha makocha mara kadhaa Erasto amekuwa chaguo la kwanza kwa kila kocha tangu ajiunge katika kikosi chetu.

Mbali nakuwa mchezaji kiraka Erasto amekuwa mchezaji kiongozi kwa wenzake kwa kuwapa ushauri kutokana na ukongwe wake.

Simba inamshukuru na kumtakia kheri Erasto katika maisha yake mapya soka nje ya kikosi chetu.

Back to homepage
Share this story