Jentrix raia wa Kenya anaondoka kikosini sio kwa sababu ya kiwango chake bali amepata timu nje ya nchi ambayo maslahi yake ni makubwa na tayari makubaliano yamefanyika.
Jentrix amejiunga nasi Julai, 2024 akitokea Beijing Queens ya China ikiwa ni mara ya pili kujiunga nasi.
Advertisement
Msimu uliopita wa 2024/2025 ameliza akiwa mfungaji bora namba mbili katika ligi kuu ya wanawake kwa kufunga mabao 26 huku akisadia kupatikana kwa mengine matatu.
Uongozi wa klabu unamtakia Kheri Jentrix katika maisha yake mapya nje ya Simba Queens huku ikimfungulia milango endapo atataka kurejea siku za baadae.