Simba Sports Club
News

Kwaheri Ismael Sawadogo

1 Jul 2023

Sawadogo raia wa Burkina Faso tumemsajili katika dirisha dogo mwezi Desemba 2022 kwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa mchezaji huru kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye eneo la kiungo wa ulinzi.

Sawadogo ameshindwa kukidhi matarajio tuliyokuwa nayo juu yake na kutokana na mipango ya timu kuelekea msimu ujao tunahitaji kuwa na kikosi bora na imara.

Baada ya kupokea ripoti ya benchi la ufundi tunaendelea kuachana na wachezaji ambao hawapo kwenye mipango ya mwalimu kabla ya kuanza kusajili wapya.

Advertisement

Mipango ya klabu ni kuhakikisha tunakuwa na kikosi bora msimu ujao kitakacho tuwezesha kuchukua mataji ya ndani pamoja na kimataifa.

Kuachana na Sawadogo ni sehemu ya maboresho ya kikosi kuelekea msimu ujao na anaungana na Augustine Okrah, Mohamed Ouattara, Victor Akpan, Gadiel Michael, Erasto Nyoni na Jonas Mkude ambao tayari tumewaaga.

Back to homepage
Share this story