Fredy alijiunga nasi msimu uliopita katika usajili wa dirisha dogo na kufanikiwa kufunga mabao tisa katika mashindano yote.
Mwanzoni mwa msimu huu Fredy alikuwa sehemu ya mpango wa timu yetu lakini kiwango chake hakikumridhisha Mwalimu Fadlu Davids na hivyo kutoa pendekezo la kusajiliwa mshambuliaji mwingine ili kuboresha safu ya ushambuliaji
Advertisement
Tayari Fredy ameshaondoka Nchini Tanzania na kuelekea Algeria kuanza majukumu yake mapya.
Uongozi wa Simba unamtakia kila la heri mchezaji huyo katika majukumu yake mapya.